Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawatangazia waombaji wote wa
mikopo wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa
masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo kuwa mwisho wa kupokea
maombi ya mikopo ni tarehe 31 Julai, 2013 na kwamba hakutakuwa na muda
wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.
Bodi
inawasisitizia waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao
hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda
uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: www.olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti:www.heslb.go.tz kabla ya tarehe 31 Julai, 2013.
Kila
mwombaji anakumbushwa kusoma kwa umakini mwongozo wa ujazaji wa fomu ya
maombi ya mikopo kwa mwaka 2013/2014 na kulipia ada ya shilingi
30,000/= kwa waombaji wapya kwa njia ya M-Pesa.
Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
No comments:
Post a Comment