EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, July 20, 2013

TAMASHA LA MATUMAINI 2013: TUNAWASHUKURU WATANZANIA.

TAMASHA la Matumaini 2013 limefanyika kwa mara ya pili Julai 7, mwaka huu kwa mafanikio makubwa ukilinganisha na lile la mwaka jana. Kwa mwaka huu limekuwa na mafanikio zaidi kwa sababu kiongozi wa juu kabisa wa nchi amepata nafasi ya kuzungumza na wananchi kuhusu amani na matumaini kwa nchi yetu.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria Tamasha la la Matumaini 2013.
Moja kati ya madhumuni mawili makubwa ya tamasha hilo ni kukumbushana umuhimu wa uzalendo wa dhati wa kudumisha amani, kurejesha matumaini kwa Watanzania waliopoteza matumaini, kuipenda na kujivunia Tanzania. 

Tunaamini kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia Watanzania, ameweza kutimiza malengo hayo kwa kiasi kikubwa.

Tunapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mhe. Rais kwa kukubali kuacha shughuli zingine na kujumuika nasi katika tamasha hilo na pia kukubali kuzungumza na wananchi na hatimaye kuandika historia mpya ya kuwa rais wa kwanza kuingia uwanjani kuanzisha mechi ya mpira wa miguu, kati ya Yanga na Simba za wabunge kwa kupuliza filimbi!

Tamasha la Matumaini limethibitisha kuwa pamoja na tofauti tulizonazo za kidini na kiitikadi, lakini sisi bado ni Watanzania ambao tunaweza kuishi pamoja na kushirikiana katika shughuli zetu za kijamii kwa amani na upendo kama ilivyojionesha katika timu za waheshimiwa wabunge, ambapo waliunda timu bila kujali tofauti zao za kisiasa.
Watanzania tunaamini tulikotoka ni mbali na tunakokwenda ni karibu, ile nchi ya matumaini, ile nchi ya neema tunayoiota kila siku imekaribia. Tunaamini baada ya miaka michache ijayo, kwa utajiri tulionao wa mafuta na gesi, Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi zenye mafanikio makubwa kiuchumi barani Afrika. Hivyo hatuna budi kuendelea kuilinda amani tuliyonayo na kudumisha mshikamano wetu.

Madhumuni ya pili ya tamasha hilo ni kutoa sehemu ya mapato yake na kuchangia Mfuko wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), ambao tangu mwaka jana, wamekuwa kwenye kampeni ya kuchangisha shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya kujenga mabweni 30 katika shule za sekondari nchini Tanzania. Hivyo Watanzania siyo tu wanapata matumaini mapya kwa kushiriki katika tamasha, bali pia wanachangia maendeleo ya elimu nchini.

Aidha, tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Watanzania wote waliobahatika kuhudhuria tamasha la mwaka huu pamoja na wale ambao hawakubahatika kufika uwanjani lakini walifuatilia kupitia runinga zao.

Katika hili tunapenda pia kuchukua nafasi hii kuishukuru TBC1 kwa kuonesha ‘live’ tamasha hilo kwani kitendo hicho kimewezesha Watanzania wengi zaidi kusikia hotuba zote mbili, ya Mhe. Rais pamoja na ile ya waandaaji halikadhalika kujionea wenyewe mechi ya wabunge wa Simba na Yanga.

Mbali ya TBC1, tunapenda pia kuvishukuru vituo vingine vya televisheni vya Channel Ten, Clouds TV, Star TV, EATV, DTV na ITV kwa kuwahabarisha Watanzania maendeleo ya tamasha, kabla na baada ya kufanyika kwake. Hakika mmefanya kazi kubwa na mmeonesha mshikamano mkubwa.

Halikadhalika shukrani za kipekee ziviendee vituo vya redio vyote hususan Times FM, Clouds FM, Radio One, Praise Power, Wapo Radio na Radio Free Africa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuwahabarisha Watanzania ujio wa Tamasha la Matumaini.

Katika orodha hiyo ya shukurani kwa vyombo vya habari, hatuna budi kuwashukuru pia wadau wenzetu kwa upande wa magazeti; Jambo Leo, Tanzania Daima, Mwananchi, Habari Leo, Nipashe, Majira, Mtanzania, Bingwa, Dimba, Spoti Leo, The Citizen na mengine yote yaliyoripoti tamasha hilo.

Tutakuwa wachoyo wa shukurani kama tutaacha kuishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na uongozi mzima wa Uwanja wa Taifa kwa kutupa ushirikiano wa kutosha na kutuamini kufanya tamasha hilo katika uwanja wao.

Pia hatuna budi kulishukuru Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam pamoja na Mkoa wa Kipolisi Temeke kwa kuimarisha ulinzi na ushirikiano mkubwa walioutoa wakati wa tamasha hilo.

Mwisho kabisa lakini ni wa muhimu sana, tunawashukuru wadhamini wetu TIGO kwa kutuunga mkono na kufanikisha tamasha kwa kiasi kikubwa. Watengenezaji wa vinywaji baridi nchini PEPSI kwa kuliunga mkono na kufanikisha tamasha hilo. Wasafirishaji wa vifurushi nchini, CDS kwa kutuunga mkono. TSN ambao ni wasambazaji wa kinywaji cha Willy Chilly na Shirika la PSI linalojishughulisha na vita dhidi ya HIV/AIDS, Malaria na magonjwa mengine nchini Tanzania.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANAZANIA
MUNGU LIBARIKI TAMASHA LA MATUMAINI
Asanteni kwa kusoma shukurani zetu za dhati kwenu. Eric Shigongo Mwenyekiti wa Tamasha
Na Abdallah Mrisho Mratibu Mkuu wa Tamasha

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate