UWEZEKANO wa Manchester United kumnasa Cesc Fabregas umeongezeka baada ya habari za kushtua kutoka Barcelona kuwa kocha Tito Vilanova (pichani) ameamua kuachia ngazi.
Kulikuwa na uvumi uliosambaa kwenye jiji la Barcelona kuwa Vilanova atalazimishwa kustaafu baada ya kupata tatizo lingine la kansa.
Mkutano wa waandishi wa habari unategemewa kuitishwa 1.30 usiku huu kwa saa za Uingereza (saa 3.30 kwa Tanzania) ambapo Rais wa Barcelona Sandro Rosell anatarajiwa kuithibitishia dunia juu ya kuondoka kwa kocha huyo.

Hiyo inamaanisha Manchester United itatumia mwanya huo kuishawishi Barcelona kumwachia Fabregas kutua Old Trafford. Tito Vilanova alionekana kuwa kizingiti ambapo juzi alikuwa mtu wa kwanza kusema Fabregas anataka kubaki Nou Camp.
Kocha mpya wa United David Moyes amekuwa na kiu ya kumnasa Fabregas na akafichua kuwa Mtendaji Mkuu Ed Woodward yuko katika maongezi na Barcelona.Inaaminika Fabregas hatakubali kuwa mchezaji chaguo la pili kwa mbadala wa Vilanova na kitendo cha Moyes kusema anataka kuijenga United kupitia Fabregas kutaongeza ushawishi.
Joan Francesc Ferrer maarufu kama “Rubi” ambaye aliteuliwa kuwa msaidiza wa Vilanova katika dirisha hili la usajili, anategemewa kuchukua nafasi ya kuliongoza jahazi la Barcelona lakini kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas naye anatajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo.
Creit: Saluti 5

No comments:
Post a Comment