Jumla
ya wanamichezo 58 wamerusha fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) utakaofanyika
Oktoba mwaka huu.
Kwa upande wa TFF waliorejesha
fomu kwa upande wa urais ni Athuman Jumanne Nyamlani,Jamal Emil Malinzi,
Omari Mussa Nkwarulo na Richard Rukambura. Nafasi ya Makamu wa Rais
wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib Ramadhan na Walace Karia.
Walioomba nafasi za ujumbe
kuwakilisha kanda mbalimbali ni Abdallah Hussein Mussa, Kaliro Samson,
Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Vedastus Kalwizira
Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko,
Stanslaus Haroon Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii.
Ahmed Msafiri Mgoyi, Yusuf
Hamisi Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja,
Ayoub Shaib Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Lugenge, Elias
Mwanjala, Eliud Peter Mvela, John Mwachendang’ombe Kiteve, James Patrick
Mhagama,
Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge.
Athuman Kambi, Francis Kumba
Ndulane, Zafarani Damoder, Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Ernest
Masima, Farid Salum Nahdi, Geoffrey Nyange, Riziki Majala, Twahil Twaha
Njoki, Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed.
Wengine ni Alex Chrispine
Kamuzelya, Juma Abbas Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir,
Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.
Kwa upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto pekee.
Kwa upande wa TPL Board
waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili tu; Hamad Yahya Juma
(Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).
Walioomba nafasi za ujumbe wa
TPL Board ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari
Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment