MKAZI wa Kijiji cha Mtungulu, wilayani Newala, mkoani Mtwara,
Kibwana Mpeme (60), amejiua kwa kuchoma moto nyumba aliyokuwamo kwa kile
kinachodaiwa kuchoshwa na maradhi ya moyo.
Taarifa zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Rashidi
Uledi, zimeeleza Mpeme aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda
mrefu, siku moja kabla ya tukio hilo aligombana na mkewe na kumpiga hadi
kumjeruhi, hali iliyosababisha apelekwe hospitali.Akizungumza kwa njia
ya simu kutoka kijijini hapo, Mohammed Mkupuni, ambaye ni mpwa wake,
Ismail Rajabu, aliyejeruhiwa akiwa katika harakati za kumuokoa
Mpeme,
alisema mke wa marehemu alipotoka hospitali alikwenda kwa ndugu yake
akihofu madhara zaidi.
Mkupuni aliiambia Tanzania Daima kuwa baada ya Mpeme kuwa peke yake
aliichoma moto nyumba aliyokuwamo na majirani walipoona moshi huku
wakijua kuna mtu ndani walianza harakati za kumuokoa.
“Ismail akiwa na wenzake waliuvunja mlango wa nyumba ili kuingia ndani
kumuokoa mzee Mpeme, lakini wakashaangaa kuona akiwalenga kwa mshale na
kumfyatulia Ismail kifuani na kumjeruhi vibaya,” alisema Mkupuni.
Aliongeza kuwa baada ya Ismail kujeruhiwa na marehemu, waokoaji
wengine wakahofia usalama wao na kususia zoezi hilo, na mzee huyo kufa
kwa kuteketea kwa moto.
Mkupuni alisema Ismail alikimbizwa hospitali kwa matibabu na polisi
kutoka Newala walifika na kuchukua maelezo ya tukio hilo na kuruhusu
mwili wa marehemu kuzikwa.
No comments:
Post a Comment