MWIGIZAJI Bongo, Kajala Masanja ambaye miezi michache iliyopita
alichomoka nyuma ya nondo za Segerea kwa dhamana, ametimkia nchini
Afrika Kusini kupunguza mawazo.
Kajala Masanja.
Mapema wiki hii, Kajala alitupia picha zake mbalimbali katika mtandao
wa Instagram zikimuonyesha akiwa nchini humo na kusindikiza na ujumbe
wa maandishi uliosomeka kuwa amekwenda kwa ajili ya kubadilisha hali ya
hewa kwani toka akumbwe na matatizo, hajapata mtoko wa kupumzisha akili.
“Nimekuja kubadilisha hali ya hewa maana nimetoka kwenye matatizo,
sijapata kabisa muda mzuri wa kuipumzisha akili yangu hivyo nimeona bora
nije huku kupumzika kidogo kisha nitarejea nyumbani,” alisema Kajala.
No comments:
Post a Comment