FILAMU ya kimataifa iliyoandaliwa Swahilihood na kwa ushirikiano wa
nchi 6 inayojulikana kwa jina la Going Bongo imekamilika mwezi wa nane,
kwa sasa watayarishaji wapo katika mikakati ya kufanya uzinduzi ambao
utatangazwa wakati wowote, akionge na FC mmoja wa watengenezaji wa
filamu hiyo Nick Marwa amesema kuwa filamu hiyo ni kazi ambayo inaweza
kuwa ni ya kwanza kwa kushirikisha watalaam kutoka nchi mbalimbali.
“Filamu ya Going Bongo ni kazi nzuri ambayo imewakutanisha watu wa
mataifa mengi kulingana na fani za filamu, lakini pia
wasanii wakubwa wa
filamu wa Tanzania na nje ya nchi wameigiza pamoja na wasanii wa ndani
ni hatua moja ya ukuzaji wa tasnia ya filamu Bongo, huku kukiwa na
changamoto ya makapuni mengine kuwekeza pesa nyingi katika
filamu,”anasema Nick.
Nchi zilizoshirikiana katika utayarishaji wa filamu hiyo ni Tanzania,
Italy, Kenya, Marekani, UK, Turkey na filamu ya Going Bongo ilianza
kurekodiwa Marekani katika jiji la Los Angeles, California na kuja
kumaliziwa Tanzania wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ni Ernest
“Napoleon” Rwandalla kinara wa filamu, Ashley Olds huyu kutoka Marekani.
Wengine ni Emanuella Galliusi kutoka Itali na Nyokabi Gethaiga kutoka
Kenya, kwa hapa nyumbani kuna waigizaji wakubwa kama Ahmed Olutu “Mzee
Chilo”, McDonald Haule, Sauda Simba Kilumang , na mtangazaji mahiri wa
Redio , Evans Bukuku ambaye pia ni mchekeshaji kutoka Redio Choice Fm.
Watayarishaji wa filamu ya Going Bongo ni Nick Marwa, Ernest
Napoleon, Bryan Ronalds, mswada umeandikwa na Ernest Napoleon Rwandallah
na Gregory Zyment wapiga picha ni mwanadada Leslie Bumgarner kutoka
Marekani akisaidiwa na George Mboya kutoka Kenya, Filamu imeongozwa na
Dean Ronalds.
Kulingana na makampuni ya usambazaji kununua filamu kwa kiwango cha
chini inawezekana ikawa ni vigumu kuweza kununua filamu hiyo ambayo
bajeti yake ya utayarishaji pekee ni milioni 450 za Kitanzania, filamu
hiyo inatarajiwa kuonyeshwa Toronto Canada na baadae katika nchi zote
washirika katika kutengeneza.
CREDIT: FILAMUCENTRAL.
No comments:
Post a Comment