ONGEZEKO la idadi ya watu katika Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke, Dar es Salaam kutoka katikati ya jiji na mikoani kunaisababishia
manispaa hiyo mzigo wa kutoa huduma.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa manispaa
hiyo, Joyce Msumba, alisema changamoto hiyo inahitaji rasilimali fedha
ili kutoa huduma za jamii.
Alisema majukumu ya Serikali za Mitaa ni kutoa huduma kwa wananchi
wake, bado kuna tatizo la wadau kushiriki katika ulipaji kodi, ushuru na
ada mbalimbali katika halmashauri hiyo.
Changamoto nyingine inayoikabili halmashauri hiyo ni ongezeko la
uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na utupaji ovyo wa takataka.
Nyingine ni ucheleweshwaji wa ruzuku kutoka Serikali Kuu, ujenzi holela wa makazi, uchache wa watendaji na vitendea kazi.
Katika hatua nyingine, alisema halmashauri hiyo imekusanya sh bilioni
25.1 katika mwaka wa fedha 2012/2013 kutoka sh bilioni 3.8 mwaka
2005/2006.
Msumba alisema fedha hizo zimetokana na vyanzo mbalimbali vya mapato yanayoizunguka halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment