JERRY SILAA, HASHEEM THABEET WAWAHUDUMIA WATU WASIOSIKIA JIJINI DAR.
Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini
Marekani Hasheem Thabeet akimpa mazoezi ya kusikia mmoja wa wagonjwa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuwekea kifaa cha
kusaidia usikivu mwanafunzi aliyetambulika kwa jina moja la Adrian jana
jijini Dar es Salaam.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahia jambo alipokuwa
akimsikiliza Mkurugenzi wa Montage Bi Teddy Mapunda (kushoto) mara baada
ya kuwasili katika eneo ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya vifaa vya
kusaidia usikivu jana jijini Dar es Salaam. Huduma hii ya kijamii ya
kusaidia watu wenye matatizo ya kusikia imekuwa ikitolewa kwa
ushirikiano wa taasisi za Starkey ya Marekani, Montage ya Tanzania na
Serena Hotel ambapo hii ni mara ya tatu tokea wameanza kutoa huduma
hiyo.
Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet akiwa na Mwanzilishi wa Starkey
ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya usikivu William Austin
alipotembelea kliniki ya kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya usikivu
hapa nchini iliyoratibiwa na Taasisi ya kusaidia usikivu (Starkey) kwa
kushirikiana na kampuni ya Montage ya Tanzania na Serena Hotel jana
jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Starkey taasisi ya kusaidia usikivu ambaye pia ni
Daktari bingwa wa magonjwa ya usikivu William Austin (wa pili kulia)
akifuatilia maendeleo ya mgonjwa wa usikivu wakati akipewa mazoezi
kufuatia kupatiwa kifaa cha kumsaidia kusikia jana jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa pili kushoto) katika
picha ya pamoja na waratibu wa kliniki ya kuhudumia watu wenye matatizo
ya kutosikia alipotembelea kliniki hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Starkey Judith Robert, Mkurugenzi
wa Montage Teddy Mapunda na Mkurugenzi wa Masoko wa Serena Hotel Serafin
Lusala.
No comments:
Post a Comment