MASTAA wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, Kajala Masanja na Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ kila mmoja amejikabidhi mtoto yatima ili amlee.
Wasanii hao walijikabidhi watoto hao nyumbani kwa Aunt Ezekiel maeneo
ya Mwananyamala jijini Dar, kulipokuwa na shughuli ya futuru hivi
karibuni ambapo Aunt aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo watoto hao wa
Kituo cha Watoto Yatima, Magomeni.
Baada ya kumaliza kufuturu, wasanii hao walijikusanya kwa pamoja na
kupiga picha na watoto hao ambapo kila msanii alichagua mtoto wake na
kuahidi kwenda kila wakati kumtembelea kituoni na kumpa huduma muhimu
kama mwanaye.
Watoto hao walipokuwa wamebebwa na mastaa hao walionekana wenye nyuso
za furaha na wakati mwingine walikuwa hawataki kushuka chini wakitaka
waendelee kubebwa na mastaa hao.
“Mimi kwa kweli nimefarijika sana kupata
mtoto mwingine ambaye atakuwa ni rafiki yangu mkubwa na nitakuwa
nakwenda kumtembelea kila wakati na hata hivi leo nilivyofuturu nao ni
faraja kubwa sana kwangu kwa vile pia mimi ni yatima,” alisema Aunt
Ezekiel.
Aunt Ezekiel akiwa na mwanaye aliyechagua kumlea.
CREDIT: GLP
No comments:
Post a Comment