Young
Africans kesho itashuka dimba la uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa
kirafiki wa kimataifa na timu ya Sports Club Villa kutoka nchini Uganda,
mchezo utakaoanza majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika
Mashariki.
Kikosi cha Young Africans kitautumia mchezo huo wa kirafiki wa
kimataifa kwa ajili ya kujiaanda na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini na pia
itakua ni sehemu ya maandalizi mchezo wa ngao ya Hisani dhidi ya Azam
FC jumamosi Agosti 17,2013.
Kocha mkuu wa Yanga Ernie Brandts mara
baada ya mazoezi ya leo amesema anashukuru kikosi chake chote
kimekamilika na kwa sasa hakuna mchezaji hata mmoja majeruhi hali
inayompa nafasi nzuri ya kumtumia mchezaji yoyote katika michezo
watakayocheza.
'Mchezo wa kesho dhidi ya Sports Club Villa ya
nchini Uganda utakua ni kipimo kizuri kwetu kesho, kwani utakua ni
mchezo wa mwisho kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom
na kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC' alisema Brandts.
Viingilio vya mchezo huo dhidi ya SC Villa ni:
VIP A Tshs 20,000/=
VIP B Tshs 15,000/=
VIP C Tshs 10,000/=
Orange, Blue & Green Tshs 5,000/=
Wapenzi
wa soka na washabiki wa klabu ya Yanga wanaombwa kujitokeza kwa wingi
kesho kuja kuiona timu ya Yanga ambayo imekamilika kuelekea kwenye
kinyang'anyiro cha kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa
2013/2014
No comments:
Post a Comment