Lori lenye namba za usajili T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka na kuziba njia
Lori likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika
Askari wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika
Dereva wa gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika kifo
YALE
YALE!!! Wananchi wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye
Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ...
bila kujali kama yaweza kulipuka
Wananchi Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka
Askari wa zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji
Wananchi mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota
Wakina mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada ya ajali
Kushoto ni Tingo Saimoni Msovela (23) na dereva wake Hassan Abdi wakijitahidi kuziba mafuta yasiendelee kuvuja
Tingo wa Lori hilo la mafuta baada ya kuokolewa kutoka kwenye Gari.
Ezekiel Kamanga
Watu wawili wamenusurika kifo baada
ya roli la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE
Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha
njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva ametambuliwa kwa jina la
HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao walikuwa wametokea DAR
ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya mafuta
Kwa mujibu wa Dereva amesema kuwa
gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko liliharibika mfumo wa breki na
mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa
makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na
kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la
tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia mlipuko wa moto ambao
ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kuchota mafuta
yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi
kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea
kuchota mafuta.
Ajali hiyo ilisababisha adha kubwa
kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa
wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.
No comments:
Post a Comment