MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, amewaagiza
viongozi wa Wilaya ya Kinondoni kuwakamata madereva wa magari na
pikipiki wanaoharibu barabara inayojengwa kwa kupitisha vyombo vyao
kwenye maeneo yasiyohusika.
Akizungumza Sadik,
alisema serikali haitavumilia kuona barabara hiyo ikiharibiwa wakati
fedha nyingi zimetumika.
Alisema viongozi hao ni lazima wasimamie sheria ipasavyo katika
kuwadhibiti watu hao ambao vitendo vyao wanavyofanya ni sawa na wahalifu
wengine.
Sadik alisema kila anayepitisha gari na pikipiki na wale wanaotumia
maeneo hayo kwa kuwasha moto wajue wanavunja sheria, hivyo ni lazima
wakamatwe mara moja.
“Watanzania ni lazima wajifunze ustaarabu wa kuthamini maendeleo yao,
pia wajue fedha zinazotumika katika ujenzi wa barabara hii na nyingine
zinatokana na kodi zao, hivyo waone uchungu kwa kuzitunza,” alisema
Sadiki.
Alitoa wito kwa viongozi wa maeneo mbalimbali ambako serikali imeamua
kuzijenga barabara zake kuhakikisha inawabaini wahalifu hao ambao
wakiachiwa wanaweza kulirudisha nyuma kimaendeleo taifa hili.
No comments:
Post a Comment