WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 14 wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Nchini (TPSF) wamemchakua Dk. Reginald Mengi kuwa mwenyekiti
mpya wa bodi ya taasisi hiyo.
Mengi alichaguliwa kuwa mwenyekiti katika uchaguzi uliofanyika
mwishoni mwa wiki ukiwa ni sehemu ya mkutano mkuu wa mwaka baada ya bodi
iliyokuwa ikiongozwa na Esther Mkwizu kumaliza muda wake.
Uchaguzi huo ulioendeshwa kwa njia ya kura ulisimamiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo.
Katika uchaguzi huo, Mengi alipata kura 39 na mgombea mwingine, Salum
Shamte alipata kura 34, hivyo kuwa makamu mwenyekiti wa bodi hiyo.
Mkutano huo mkuu pia uliwachagua wajumbe 11 walioomba uongozi kupitia kongano wanazotoka ili kuwa wajumbe wa bodi hiyo.
Baada ya kutangazwa mshindi, Mengi alisema katika kipindi chake
atashirikiana na bodi na sekretarieti ya TPSF kuhakikisha yale yote
mazuri yaliyofanywa na uongozi uliopita yanaendelezwa.
Alitoa changamoto kwa serikali kutumia fursa za rasirimali zilizopo
nchini kwa kuwapa kipaumbele Watanzania kwa ajili ya maslahi zaidi ya
nchi kama zilivyofanya nchi za Korea Kusini na Malasia.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, alisema taasisi hiyo
imepata kwa mara nyingine viongozi mahiri katika nyanja ya masuala ya
biashara na wenye ushawishi katika kuzungumza na serikali.
No comments:
Post a Comment