MWANAFUNZI wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Sokoine,
Manispaa ya Dodoma (jina linahifadhiwa), anadaiwa kuwekwa kinyumba na
mwalimu wake David Macha (30).
Mwanafunzi huyo wa miaka 14 ni kati ya watoto wanaofadhiliwa na
shirika kisilo la kiserikali la Compassion International Tanzania kituo
cha Tz 807 FPCT kilichoko Chamwino.
Hata hivyo, katika hali kushangaza Jeshi la Polisi mkoani hapa,
limelalamikiwa na wazazi wa mtoto huyo kwa kitendo cha kumlinda
mtuhumiwa licha ya kupewa taarifa za uhalifu huo kwa zaidi ya miezi
mitano sasa, limeshindwa kumchukulia hatua.
Uchunguzi ambao umethibitishwa na wazazi wa
mwanafunzi huyo, umebaini kuwa mwalimu Macha amekuwa akifanya mapenzi na
mwanafunzi huyo kwa zaidi ya miezi mitano sasa.
Wazazi wa mwanafunzi huyo wanathibitisha kuwa kwa zaidi ya miezi
mitano, mtoto wao alikuwa na tabia ya kutoroka nyumbani nyakati za
usiku na kulala nje, jambo ambalo lilianza kuwatia mashaka na kuanza
kufuatilia nyendo zake.
CREDIT: Tanzania Daima.
No comments:
Post a Comment