Siku chache baada ya kupona madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya
‘unga’ midume kibao imejitokeza kuwania kumuoa staa mkubwa wa muziki wa
Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Ishu
hiyo ilianza tangu mwanadada huyo maarufu kama Kiuno Bila Mfupa
alipohojiwa kupitia CloudsTV ambapo alieleza jinsi alivyofiti kiafya.
“Unajua
tangu aliposema anamshukuru Mungu kumuepusha na shetani wa madawa ya
kulevya, wanaume kibao wamekuwa wakimfuatilia wakitangaza dau la kumuoa.

“Kama
hamuamini fuatilieni akaunti yake kwenye Instagram (mtandao) muone.
Kila akiweka picha mpya kwa ajili ya mashabiki wake kinachofuata ni
maombi ya wanaume wanaomsifia kuwa ni mzuri.

Chanzo chetu kilipoperuzi kwenye akaunti hiyo ya Ray C na kukutana na maombi hayo ya wanamme.
Katika
mahojiano yake na CloudsTV, Ray C alisema kwa sasa hawazi kitu kingine
tofauti na kurudi kwanza kwenye muziki kwa kishindo.
No comments:
Post a Comment