Mwanamke wa kitanzania mwenye umri wa miaka 34, wiki
iliyopita alikamatwa katika kiwanja cha kimataifa cha Harare baada ya kukutwa na dawa haramu zenye
thamani ya dola 45,000 kwa bei za mtaani alipowasili kutoka India.
MWANDISHI MWANDAMIZI
Jackline Mollel Richard,
ambaye anaishi Afrika Kusini, hakuambiwa ajitetee alipokuwa mbele ya hakimu wa
Harare Donald, Ndirowei . Aliwekwa rumande chini ya ulinzi hadi Julai 27
Jackline amekutwa na milki ya kilo 15 ya efedrini ambayo inasaidia kushitua mfumo wa moyo na mfumo wa neva. Ni mara nyingi hupatikana katika dawa za
mitishamba na chakula.
Inasemekana kuwa Jackline
aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare na ndege ya Emirates
kutoka India . Alitoa passport yake katika meza ya uhamiaji na ndipo afisa tahadhari
alipowatonya wapelelezi wa madawa ya kulevya kwamba mama huyo ana viza ya India
ambayo ni chanzo maalumu kwa ajili ya madawa haramu.
mahakama ilipata taarifa kuwa Jackline alichukuliwa kwa
ajili ya kuhojiwa na wakati anakaguliwa na wapelelezi hao alikutwa na bahasha
30 za khaki ikiwa na vitu vyeupe ambayo vilikuwa vimefungwa pamoja na kitambaa ndani ya beg la maruni.
Vipimo vilifanyika kwenye bahasha hizo na ikabainika kuwa ilikuwa efedrini. Madawa ya kulevya hayo yalichukuliwa kwa ajili ya kurekodiwa na kupima uzito.
No comments:
Post a Comment