MAHAKAMA ya Rufaa imetupilia mbali maombi ya rufaa ya kupinga
hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza,
iliyowatia hatiani Shija Madata na wenzake wawili kutumikia kifungo cha
miaka 55 jela baada ya kumfanyisha ngono mtoto na mbwa.
Rufaa hiyo ilitupiliwa mbali na jopo la majaji watatu; Natharia
Kimaro, Ibrahimu Juma wakiongozwa na Jaji Januari Msofe, wakisema hoja
za warufani hazikuwa na mashiko ya kubatilisha hukumu ya awali.
Akisoma hukumu hiyo jana kwa niaba ya jopo hilo, Naibu Msajili wa
Mahakama ya Rufani, Bampikya Willibard, alisema baada ya majaji kupitia
hoja za warufani walibaini hazina mashiko kulingana na kosa walilotenda.
Alisema kuwa waomba rufaa walitenda kosa baya. Kwamba mbali na
kumshushia hadhi mwathirika wa tukio hilo, kulikuwa na mazingira ya
kumsababishia magonjwa.
Alifafanua kuwa waliamuliwa kulipa kila mmoja fidia ya sh 200,000 na
wataendelea kutumikia kifungo jela kama ilivyoamuliwa na mahakama ya
mkoa.
Shija ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 18, kwa pamoja na
wenzake walipatikana na hatia katika kesi ya kumlazimisha mtoto wa miaka
13 kufanya ngono na mbwa.
Mbali na Shija, warufani wengine ni Job Mlama, ambaye wakati huo
alikuwa na miaka 30 na Anicet Edward, aliyekuwa na miaka 30,
ambao walihukumiwa kifungo cha miaka 40 kila mmoja baada ya kupatikana
na hatia katika kesi hiyo.
Warufani walihukumiwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Gadiel
Mariki, baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi na kuwaona
walikuwa na hatia kutokana na shitaka lililokuwa likiwakabili.
Kwamba kitendo walichokifanya kilikuwa cha kinyama na hakikustahili
kuvumiliwa kwenye jamii iliyostaarabika kama Tanzania, hivyo akatoa
adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Shija anatumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kumrubuni mtoto
na kumpeleka kwenye kambi ya madini ya Barrick kwa nia ya kumfanyisha
ngono na mbwa.
Hakimu Mariki katika hukumu hiyo alisema katika kosa la pili
watuhumiwa Shija, Job na Anicet watatumikia kifungo cha miaka 20 kila
mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumshawishi mtoto kukaa maeneo ya
kambini na kumfanyisha ngono na mbwa.
Kwamba wote watatu watatumikia jela miaka 20 mingine kwa kosa la kumlazimisha kwa nguvu mtoto kufanya ngono na mbwa.
Mbali na adhabu hiyo kwa washtakiwa, Hakimu Mariki aliagiza wamiliki
wa mgodi wa Barrick kumkabidhi mbwa huyo mikononi mwa Jeshi la Polisi
mkoani Mwanza ili amilikiwe na serikali.
Hata hivyo alisema kuwa watuhumiwa hao watazitumikia adhabu hizo kwa
pamoja, hivyo watakaa jela miaka 20 kila mmoja na kusisitiza kuwa kama
hawakuridhishwa na uamuzi wa mahakama hiyo wana haki ya kukataa rufaa.
Wakili Mfawidhi wa Serikali, Edwin Kakoraki, wakati huo, aliiambia
mahakama kuwa tukio hilo lilifanyiika Machi 21, 2008, ambapo watuhumiwa
hao walikuwa kwenye kambi ya utafiti wa madini ya Barrick wilayani
Sengerema.
Kwamba walimlazimisha mlalamikaji ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa
la tatu katika Shule ya Msingi Sota kufanya ngono na mbwa, ambapo siku
ya tukio mlalamikaji alikwenda kwenye kambi hiyo akiwa na Shija ambaye
ni rafiki yake baada ya kumfuata nyumbani kwao saa 1:00 usiku na
kumuomba amsindikize kwa rafiki yake wa kiume, aliyekuwa mshitakiwa
namba moja Job Mlama.
Mahakama ilielezwa kuwa Shija na mlalamikaji walipofika kwa Job,
walipewa chakula na kisha maji ya kuoga, baadaye Shija alijilaza
kitandani kwa Job na ilipofika saa 4:00, Shija na Job walimwambia
mlalamikaji waende kwenye chumba kingine wakazunguke kisha watarudi.
Ilidaiwa kuwa mlalamikaji alikubaliana na kauli ya rafiki yake, hivyo
kuondoka wote watatu na kuelekea kwenye nyumba ambacho Shija na Job
walikuwa wakimpeleka mbwa na walipofika kwenye banda la mbwa walimkuta
Anicet ambaye ni mwangalizi wa mbwa.
Ilidaiwa kuwa watuhumiwa wote watatu walishirikiana kumvua mlalamikaji
nguo zote na kumsukumia kwa mbwa dume mwenye rangi nyeusi na Anicet
kumuonyesha ishara mbwa huyo ambaye alianza kumwingilia mlalamikaji.
Kwamba wakati mbwa huyo ikimwingilia kinyume cha maumbile, mlalamikaji
alikuwa akipiga kelele kuomba msaada lakini washitakiwa wote watatu
walikuwa wakicheka na kushangilia.
No comments:
Post a Comment