STAA wa filamu za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ kwa mara nyingine
tena amekumbwa na tuhuma za kukwepa kulipa deni la shilingi 400,000
analodaiwa na staa mwenzake, Husna Iddi ‘Sajenti’, Amani linakujuza.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Koleta alikopa nguo kwenye duka la
Sajenti kwa maelezo kwamba angelipa jioni ya siku hiyo lakini mpaka sasa
ni miezi saba imepita bila msanii huyo kulipa deni hilo.
Ikazidi
kudaiwa kuwa hata Sajenti anapompigia simu Koleta ili kumuulizia kuhusu
deni hilo, msanii huyo hapokei simu, hali inayotoa tafsiri kwamba
anataka kumdhulumu.
Paparazi wetu alimtafuta Sajenti ili kupata uhakika kama kweli anamdai Koleta ambapo alifunguka kama ifuatavyo:
“Sijawahi kumuona mtu msumbufu kama Koleta na sasa naanza kuamini maneno ya watu kwamba ana asili ya utapeli,” alisema Sajenti.
Akaongeza kuwa anamdai Koleta tangu mwaka jana na imefikia hatua sasa hapokei simu yake.
“Kinachoniuma
ni pale anaposhindwa kupokea simu yangu, nikitumia simu asiyoijua
anapokea na akijua ni mimi ananipa ahadi za uongo,” alisema Sajenti.
Paparazi
wetu alimsaka Koleta na kumsomea tuhuma zake ambapo alikubali kudaiwa
na Sajenti ila akakanusha kutopokea simu zake, akadai kwamba ameshaongea
na msanii huyo ili alipe deni hilo kwa awamu.
Credit:GLP
No comments:
Post a Comment