Dar es Salaam.
Wanafunzi wametakiwa kusoma kwa bidii na kuamini kuwa miongoni mwao wote wanaweza kushika nafasi za juu katika masomo hivyo kuweza kutimiza ndoto zao za kuwa watu wenye mafanikio maishani.
Wanafunzi wametakiwa kusoma kwa bidii na kuamini kuwa miongoni mwao wote wanaweza kushika nafasi za juu katika masomo hivyo kuweza kutimiza ndoto zao za kuwa watu wenye mafanikio maishani.
Akizungumza wakati wa mahafali ya saba ya wanafunzi wa darasa la saba katika Shule za Sunrise Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi alisema watoto wote wana nafasi sawa ya kuweza kufanya vizuri darasani kinachotakiwa ni kujiamini.
“Pia mnatakiwa kusoma kwa bidii kwani hakuna miujiza katika jambo hilo hivyo mnahitaji jitihada binafsi” alisema na kuongeza kuwa wazazi na wanajamii wengine wametakiwa kuwa karibu nao na kuwasaidia kitaaluma kadiri inavyowezekana.
Mengi alibainisha kuwa watoto bila msaada wa
wanajamii wengine ni vigumu sana kuweza kufanikiwa maishani hivyo
mchango wao una nafasi kubwa kuwafanya watoto watimize ndoto zao pia
amewataka wadau mbalimbali kujitokeza na kuwekeza zaidi katika suala la
elimu.
Katika hafla hiyo ambayo ilipambwa na mashairi, ngoma na sanaa zingine ziliozoonyeshwa na watoto hao, Mkuu wa shule hiyo , Onesphor Vitalis alisema wazazi wanatakiwa kutambua majukumu yao kwa kufuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto wao ili kufanya mtiririko wa masomo uwe na uwiano.
Alisema mzazi au mlezi kukagua kazi za mwanaye na
kumsaidia kitaaluma kunamjenga mtoto na kumfanya ahisi kuwa kile
anachokifanya kina baraka za wazazi.
na sio kuachiwa jukumu hjilo walimu pekee.
No comments:
Post a Comment