MSHAMBULIAJI Didier Drogba ameendelea
kuwa mwiba kwa Arsenal akikumbushia enzi zake alipokuwa na jezi ya
Chelsea, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 siku ya jana kufunga
mabao mawili na kuiwezesha klabu yake, Galatasaray kutwaa Kombe la
Emirates.
Kweli, ni mashindano ya kirafiki na
hayana maana yoyote katika msimu, lakini lilikuwa kama pigo lingine kwa
kikosi cha Arsene Wenger.
Mfaransa huyo aliwaka ile mbaya kana
kwamba mashindano hayo yana maana yoyote.

Amefunga: Drogba amefunga mabao dakika za lala salama Kombe la Emiratesjana.

Kitu nyavuni: Drogba akimuuza Wojciech Szczesny
Alimfokea refa wa akiba, Andre
Marriner baada ya refa Jon Moss kuwazawadia penalti wapinzani dakika 12
kabla ya filimbi ya mwisho kutokana na Ignasi’s Miquel kumsukuma
mshambuliaji huyo wa Ivory Coast.
Drogba alikwenda mwenyewe kupiga penalti hiyo na kumpeleka upande tofauti kipa Wojciech Szczesny na mpira alipoupiga.
Drogba akafunga tena zikiwa zimesalia dakika nne, baada ya kupokea pasi ya Wesley Sneijder na kumuacha Per Mertesacker, kabla ya kumtungua tena Szczesny.
Arsenal ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo dakika ya 38, mfungaji Theo Walcott.
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Gibbs/Miquel dk69, Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla/Zelalem dk61, Walcott na Sanogo/Giroud dk61.

Mnanikumbuka? Drogba akishangilia baada ya kufunga bao la pili

La kwanza: Walcott akishuhudia krosi yake ikiipa Arsenal bao la kuongoza

Walcott akishangilia na wachezaji wenzake wa Arsenal

Amerudi nyumbani: Emamanuel Eboue (kulia) alikuwa Nahodha wa Galatasaray ilipomenyana na timu yake ya zamani leo, Arsenal

Mtu mpya: Yaya Sanogo ameng'ara katika michuano yake ya kwanza ya Kombe la Emirates

Johan Elmander wa Galatasaray akipambana na Kieran Gibbs wa Arsenal

Kadata na kichapo: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alivyokuwa baada ya kipigo
No comments:
Post a Comment