Dar es Salaam.
Wakati Kampuni ya Azam Media na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zikisaini rasmi mkataba wa kuonyesha Ligi Tanzania Bara, Klabu ya Yanga imeshangazwa na hatua hiyo ikisema imefanyika kinyume na mapendekezo yake.
Wakati Kampuni ya Azam Media na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zikisaini rasmi mkataba wa kuonyesha Ligi Tanzania Bara, Klabu ya Yanga imeshangazwa na hatua hiyo ikisema imefanyika kinyume na mapendekezo yake.
Awali, pande hizo mbili ziliingia mkataba wa makubaliano kabla ya jana kusaini mkataba rasmi.
Katika mkataba huo, kila klabu itaweka kibindoni kitita cha Sh100 milioni kutoka Azam Media, ambayo itakuwa inaonyesha ‘Live’ mechi za Ligi Kuu kupitia Azam TV.
Hata hivyo, mkataba wa makubaliano kati ya Azam
Media na TFF ulipingwa na klabu ya Yanga, ambayo ilidai ulikuwa na
upungufu na kuomba upitiwe upya kabla ya kusainiwa mkataba rasmi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo, Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani alisema, fedha zitakazotolewa na Azam Media zitazisaidia klabu kutekeleza mipango ya maendeleo.
“Soka haliwezi kuendeshwa kwa viingilio, mkataba huu utazisaidia klabu kutekeleza mipango ya maendeleo sambamba na kuifanya ligi yetu iwe bora,” alisema Nyamlani.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence
Mwalusako alisema ameshangazwa na uamuzi wa Azam Media na TFF kusaini
mkataba wakati mapendekezo yao hayajafanyiwa kazi.
“Taarifa za kusaini mkataba nimezisikia leo asubuhi, kweli zimenishangaza. Makubaliano yalikuwa, bodi ya Ligi na Azam ziupitie upya kisha mwanasheria wetu auone ndiyo mambo mengine yafuate,” alisema Mwalusako.
Aliongeza: “Siwezi kulizungumzia sana hili, lakini
ndiyo yalikuwa makubaliano yetu sasa kama wamesaini bila mapendekezo
yetu kufanyiwa kazi ni jambo linaloshtua.”
No comments:
Post a Comment