Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, jana ulimnasa 'Daktari Feki' aitwaye Alex Sumni Massawe (33).
Massawe alikamatwa saa 5:00 asubuhi ndani
ya hospitali hiyo na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi
la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa
amepanga kumfanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa
na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia
huduma kwa malipo ya Sh. 200,000.
Habari zinasema kuwa kabla ya kukamatwa kwa
Alex, mama mzazi wa kijana huyo, mkazi wa Manispaa ya Moshi, Pamvelina
Shirima, alikutana na mtuhumiwa huyo katika baa moja maarufu iliyopo
eneo la Dar Street (jina limehifadhiwa) na kumtaka ampe kiasi hicho cha
fedha kwa madai zitatumika kuharakisha mwanaye wa kiume kufanyiwa vipimo
vya upasuaji.
Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo,
alisema kuwa daktari huyo aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo
baada ya baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mtu ambaye amekuwa
akijitangaza kwamba ni daktari.
PICHA: MICHUZI BLOG
PICHA: MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment