Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiongea na Afisa Mwandamizi
mradi wa FHI 360 Road II Bi Florence Lema na Mratibu wa Mradi eneo la
Sumbawanga Ndugu Nsajigwa Richard walipofika ofisini kwake siku ya jana kushukuru
kwa msaada wa ofisi waliopewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambayo
waliitumia kwa muda wa miaka mitatu.
Afisa Mwandamizi mradi wa FHI
360 Road II Bi Florence Lema akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa
Alhaj Salum Mohammed Chima barua ya shukurani kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
huo kuwasaidia Ofisi waliyoitumia kwa mda wa miaka mitatu katika kipindi
chote cha mradi ambao ambao hivi sasa umekamilika.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akionyesha barua hiyo
mara baada ya kukabidhiwa ofisi iliyokuwa ikitumika na mradi wa FHI 360
Road II Mkoani Rukwa. Afisa Mwandamizi wa mradi huo Bi. Florence Lema
ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano Mkubwa
ilionao katika kusaidia na kujumuika pamoja na sekta binafsi na
mashirika ya kijamii ya kitaifa na kimataifa.
Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na wawakilishi kutoka FHI 360 Ofisi kwake mapema siku ya jana.
No comments:
Post a Comment