MAHAKAMA Kuu ya Tanzania kanda ya Songea mkoani Ruvuma imeanza
vikao vyake katika vituo viwili tofauti Songea na Mbinga ambapo kesi 37
za mauaji zitasikilizwa.
Msajili wa wilaya mahakama kuu Tanzania kanda ya Songea Wilfred
Nyansobera alisema kati ya kesi hizo zitakazosikilizwa zipo ambazo
maelezo ya awali na ushahidi utasikilizwa.
Nyansobera alisema kikao cha kwanza kitaendeshwa na Jaji Patricia
Fikirini akisaidiana na wakili mkuu mfawidhi wa serikali kanda ya Songea
Andikalo Msabila na wakili wa kujitegemea Christandus Komba na Frank
Ngafumika.
Alifafanua kuwa katika kikao hicho cha kwanza jumla ya kesi 16
zimepangwa ikiwa 12 zitasikilizwa maelezo ya awali na nne zitasikilizwa
ushahidi.
Alisema kikao kingine kitaendeshwa na Hakimu Mkazi Mkuu Wilfred
Dyansobera akisaidiana na wakili wa serikali Okoa Mgavilenzi na wakili
wa kujitegemea Dickson Ndunguru ambapo kesi 10 zimepangwa ikiwemo nne za
wauaji kwa ajili ya kusikiliza ushahidi na sita rufaa za jinai.
Kikao kingine kinaendeshwa Mbinga na Jaji mfawidhi kanda ya Songea
Mwanaisha Kwariko ambapo jumla ya kesi 11 zimepangwa ikiwa kesi tano za
mauaji zitasikilizwa ushahidi na kwamba kesi tatu ni za rufaa za jinai
huku zingine tatu zikiwa ni maombi na rufaa ya kesi za madai.
No comments:
Post a Comment