RAIA wawili ndugu wa Kenya, Mark Rubila (16) na Sila Rubila (21)
wanaodaiwa kumuua dereva teksi, Ramadhani Mahembe (38) mkazi wa
Buguruni Chama, wameanza kufichua siri mbalimbali kuhusu matukio
mbalimbali ya ujambazi ambayo wamekuwa wakiyafanya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi, Wakenya hao
kutoka mji wa Kakamega wameshafanya matukio mengi ya ujambazi yakiwamo
ya uporaji magari.
“Wahenga wanasema siku za mwizi ni arobaini, hivyo ndivyo
inavyodhihirika kwa Wakenya hao ambao wamefichua siri zaidi kuhusu
ujambazi waliokuwa wakiufanya na kueleza kuwa gari walilotaka kumpora
marehemu Mahembe walitaka kulipeleka mkoani Tanga kwa mteja.
“Hao vijana ni wadogo kiumri lakini wanaonesha ni hatari sana kwani
wameeleza kuwa wameshafanya matukio mengi yakiwamo ya kuiba magari
mengi, walipoulizwa ilipo Toyota Hilux walisema walilificha sehemu
mkoani Tanga,” kilieleza chanzo kingine.
Baada ya kubanwa zaidi inadaiwa kuwa watuhumiwa hao waliwaeleza polisi
kuwa awali walimpelekea mteja gari aina ya Toyota Hilux na alilikataa
na kuwaeleza kuwa anataka gari dogo.
Chanzo hicho kinadai kuwa watuhumiwa hao walitaja watu kadhaa ambao wamekuwa wakishirikiana nao.
Siku za hivi karibuni matukio ya ujambazi yamekuwa yakiliandama Jiji
la Dar es Salaam mfululizo kwa benki za watu binafsi kuporwa mamilioni
ya fedha.
No comments:
Post a Comment