Klabu ya Manchester United imemsaini Marouane Fellaini kutoka Everton kwa Pauni Milioni 27.5.
David Moyes ameungana na kijana wake wa zamani baada ya
kumfukuzia kwa muda mrefu, akibebwa na maombi yake ya mapema kwa
mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ubelgij.
Mwishowe United wamekata kiu kwa kumpata
mchezaji waliyekuwa wakimtaka, ingawa wamelipa Pauni Milioni 3.5 zaidi
kutoka walizotoa kumnunua Robin van Persie msimu uliopita.
Kiungo huyo wa Ubelgiji, Fellaini
amekuwa akitakiwa kuungana na kocha wake wa zamani, Moyes na hakuwa na
chaguo zaidi, isipokuwa kutua United.
Fellaini amepewa ruhusa ya kuchelewa
kujiunga na kikosi chake cha timu yake ya taifa, ili kukamilisha
uhamisho wake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutua United, ambao
ulikuwa unashughulikiwa na baba yake, Abdellatif.
United ilituma ofa tofauti kwa wote
Fellaini na Leighton Baines mapema majira haya ya joto, ikianza na Pauni
Milioni 28 jumla kwa wote na baadaye Milioni 36, ambazo zote zilipigwa
chini na Everton.
Na inafahamika kwamba United ilijaribu
kumsajili Mesut Ozil aliyetua Arsenal kwa Pauni Milioni 42 kutoka Real
Madrid na ilitoa ofa iliyodunda na Pauni Milioni 34 kwa mchezaji
mwingine wa Real, Sami Khedira kabla ya kujaribu kwa nyota wengine wa
klabu hiyo Luka Modric bila mafanikio.

Wameungana tena:Kocha wa Manchester United, David Moyes alifanya kazi na Fellaini alipokuwa Everton


walengwa: Wote Fellaini (kushoto) na Leighton Baines (kulia) waliichezea Everton huko Cardiff Jumamosi
No comments:
Post a Comment