KOCHA Manuel Pellegrini jana alikuwa
mwenye furaha baada ya timu yake, Manchester City kuanza vyema Ligi ya
Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya wenyeji Viktoria Plzen katika kundi lao D lenye timu za Bayern Munich na CSKA Moscow.
Dakika
10 zilitosha kwa City kutengeneza ushindi mnono na sasa wanaelekea
kwenye mchezo na mahasimu, Man United Jumapili wakiwa wenye kujiamini.
Edin
Dzeko alifunga la kwanza dakika ya 48, Yaya Toure akafunga la pili
dakika ya 53 na Sergio 'Kun' Aguero akakamilisha kazi dakika ya 58 kwa
bao la tatu.
Kikosi
cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov,
Toure (Javi Garcia 80), Fernandinho, Jesus Navas/Milner dk67, Aguero,
Nasri, Dzeko/Negredo dk83.
Plzen:
Kozacik, Rajtoral, Hejda/Hubnik dk66, Prochazka, Limbersky, Horava,
Horvath, Petrzela, Kolar/Duris dk61, Kovarik, Bakos/Tecl dk84.

Salamu United: Wachezaji wa Manchester City wakishangilia ushindi wao wa ugenini dhidi ya Viktoria Plzen

Mwanzo mzuri: Wachezaji wa Manchester City wakisherehekea kuanza vyema Ligi ya Mabingwa

La kwanza: Edin Dzeko aliifungia bao la kwanza Manchester City


Huwezi kuzuia mchomo huu: Kipa wa
Viktoria Plzen, Matus Kozacik akirukia mpira uliopigwa na kiungo wa
Manchester City, Yaya Toure (hayupo pichani) bila mafanikio, unapita
kutinga nyavuni

Yaya Toure akishangilia baada ya kufunga bao zuri kutoka nje ya boksi

Samir Nasri akimtoka mchezaji wa Viktoria Plzen, Lukas Hejda


Vitani: Sergio Aguero akipambana na Lukas Hejda

Aguero akishangilia baada ya kufunga bao la tatu


Aguero akishangilia na Dzeko, na Toure na Nasri

Mwanzo mzuri: Manuel Pellegrini alifurahia ushindi wa ugenini jana
No comments:
Post a Comment