Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akikagua kiwanda cha maji cha
Dew Drop kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndani Ndugu Aziz Tawaqal
alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa tarehe 18 Sept 2013. Kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj
Salum Mohammed Chima.
Kiwanda cha kisasa cha Dew Drop
chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 6,000 kwa saa yakiwa na ubora wa
hali ya juu. Maji hayo huzalishwa katika hali ya usafi na hayaongezwi
kemikali yeyote ambapo husafishwa kupitia "Sand Filters", "Activated
Coal" na teknolojia ya "UV Light".
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji
ya Dew Drop Aziz Tawaqal akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi alipofika kiwandani
hapo kujionea shughuli mbalimbali za muwekezaji huyo ikiwemo kiwanda cha
unga cha Energy Milling.
Waziri Lukuvi akipokea maelezo ya
Maji ya Dew Drop kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji ya Dew
Drop Aziz Tawaqal, Waziri huyo aliyasifia maji hayo na kusema kuwa
ameyanywa na ni mazuri sana ukilinganisha na maji mengine yanayozalishwa
hapa nchini.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
No comments:
Post a Comment