EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, September 24, 2013

MJANE MWEUPE...MWANAMKE ALIYEONGOZA SHAMBULIO LA KIGAIDI KENYA,MATUKIO ALIYOHUSIKA

-Aliwahi kuja Tanzania akiwa na wanaye watatu
-Alikuwa mke wa Lindsay, mtuhumiwa wa ugaidi jijini London
-Alikuwa anatafutwa na polisi wa Kenya kabla ya tukio la juzi
-Al-Shabaab wamtaja kuwa mwanamke shujaa
-Alipanga kumtorosha mwenzake aitwaye Grant leo

Samantha Lewthwaite Mjane Mweupe' anayedaiwa kuhusika katika shambulio la Nairobi.
Baadhi ya majeruhi katika shambulio la kigaidi jijini Nairobi.

Habari: Clarence Mulisa na Mitandao
MWANAMAMA Samantha Lewthwaite amehusiswa katika shambulio la kigaidi lililotokea jijini Nairobi, juzi Jumamosi kwenye jengo la biashara la Westgate.

Lewthwaite amehusiswa kuwa miongoni mwa magaidi 10-15 wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo lililopoteza maisha ya watu 69 mpaka sasa wakati zaidi ya 175 wakijeruhiwa.
Mume wa Lewthwaite, Germaine Maurice Lindsay aliyeuawa watu 26 katika mlipuko wa Julai 7, 2015 jijini London.

Samantha Lewthwaite (29), maarufu kama 'Mjane Mweupe' ni Mwingereza aliyekuwa mke wa Germaine Maurice Lindsay maarufu kwa jina la Abdullah Shaheed Jamal, mmoja wa magaidi kati ya wanne waliojitoa mhanga katika shambulio la Julai 7, 2005 jijini London lijulikanalo kama (7/7) lililouwa watu 56 pamoja na wao na kujeruhi zaidi ya 700.
Bomu la Lindsay liliua watu 26 baada ya kulipua treni ipitayo chini ya ardhi jijini London.
Lewthwaite, ambaye alibadili dini enzi za ujana wake na kuitwa Sherafiyah anadaiwa kuwa na watoto watatu.

Serikali ya Kenya imeeleza kuwa baadhi ya majeruhi waliookolewa kutoka katika jengo la Westgate walidai kumuona mwanamke mweupe (aliyefanana na Lewthwaite) akiwa miongoni mwa magaidi walioteka jengo hilo.
Mabaki ya treni iliyolipuliwa na Germaine Lindsay na kuuawa watu 26.

Al- Shabaab kupitia katika akaunti yao ya Twitter wamemtukuza Lewthwaite kwa kusema yupo katika viwango vyao na ni mwanamke shujaa.

Inasadikiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa mmoja kati ya viongozi wa magaidi hao baada ya askari kudai kuwa mwanamke mweupe aliyekuwa amevaa hijabu alikuwa akitoa amri kwa wenzake katika lugha ya Kiarabu wakati wa shambulio hilo.

Desemba 2011, askari nchini Kenya walibaini kemikali za kutengeneza milipuko sawa na zile zilizotumika katika milipuko ya Julai 7, 2005 jijini London katika vyumba viwili vya kupangisha. Lewthwaite alidaiwa kuwa ndiye aliyekuwa amepangisha vyumba hivyo japo hakukamatwa.

Katika tukio hilo, Mwingereza, Jermaine Grant, alikamatwa akiwa jijini Mombasa kwa kuhusika na kemikali hizo. Baada ya kukamatwa, Grant aliwaeleza askari wa Kenya kuwa anafanya kazi chini ya Lewthwaite. Alikamatwa pamoja na mtu mwingine aliyekuwa anajaribu kutoroka nchini Kenya.
Habari iliyotolewa na gazeti la The Sun la Septemba 23, 2005 ikiwa na picha ya Lewthwaite akiwa amembeba mwanaye wa kike Ruqayyah, aliyezaa na Linsday.

Februari 2012, iliripotiwa kuwa mwanamke aliyekuwa akitumia vitambulisho mbalimbali kikiwemo cha Lewthwaite alikuwa anatafutwa na polisi wa nchini Kenya, baada ya kugundulika hati feki ya kusafiria ya Afrika Kusini iliyokuwa na picha yake katika nyumba iliyohusishwa na vitendo vya kigaidi.

Aprili 2012, ilithibitishwa kuwa mtuhumiwa katika tukio hilo alikuwa Lewthwaite mwenyewe ambaye anadaiwa kuvuka mpaka wa Kenya na kuja Tanzania akiwa na watoto wake watatu Desemba 26, 2011.
Watoto wakiwa eneo lililoshambuliwa na magaidi.

Machi mwaka huu, Daily Telegraph liliripoti kuwa Lewthwaite na Fouad Manswab walikuwa wanapanga kumtorosha Grant na mpango wao ulipangwa kufanyika leo Septemba 23, 2013 jijini Mombasa.
 
"Tunajua Fouad anawasiliana na Samantha Lewthwaite na walipanga kumuokoa mwenzao," alisema Jacob Ondari, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wa Kenya kipindi hicho.

Katika ripoti mbalimbali, Lewthwaite anatajwa kuwa mfadhili, muongozaji na mwalimu wa al Qaeda na muandaaji wa Kundi la Jihad kwa wanawake barani Afrika.

Habari kwa hisani ya GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate