Msanii
 wa Hip hop, Nick wa Pili akiwapanua mawazo wakazi wa Morogoro na kuwapa
 mbinu zaidi za kutumia fursa zilizopo mkoani hapo.
 Meneja Ujasiriamali wa Zantel, Haidar Chamshama, akiwaonyesha wakazi wa
 Morogoro namna ya kutumia fursa ya kubana matumizi kwa upande wa 
utumiaji wa simu za mkononi na kujua faida za simu zaidi katika 
kujikwamua kimaisha.
Mkuu
 wa Utafiti wa Maxcom Africa, Ahmed S Lussasi, akiwafafnulia wakazi wa 
Morogoro namna wanavyoweza kufaidika na bidhaa za Maxcom katika 
kujikwamua kimaisha.
 Mtangazaji wa Kipindi cha Sport Extra cha Clouds FM, Shaffih Dauda akionyesha namna ya kutumia  fursa kwa upande wa michezo.
Mbunifu
 wa Mavazi wa Morogoro, Diana Magesa (kushoto), akizungumzia fursa ya 
mambo ya ubunifu, huku akionyesha mavazi yake kwa kumvisha Mtangazaji wa
 kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM,  Jelard Hando, ambaye 
alikuwa mshereheshaji wa semina hiyo.  
 Mtalaam wa mambo ya Kilimo, Yona Joram, akiwafafanulia namna ya kutumia fursa kwenye upande wa kilimo.
 Mwakilishi
 wa NSSF kutoka Makao Makuu, Salim Khalfani akizungumzia namna ya 
kutumia fursa zinazotokana na mafao ya NSSF kwa wakazi wa Morogoro leo 
ndani ya ukumbi wa Midland Hoteli mjini Morogoro.
 Ruge
 akihitimisha Semina hiyo kwa kukaribisha maswali kutokana na mafunzo 
waliyoyapata wakazi wa Morogoro waliohudhuria kwenye semina ya Kamata 
Fursa Twenzetu mapema leo.
 Baadhi
 ya wakazi waliokuwa ndani ya ukumbi huo wakiwa wamesimama baada ya 
kuombwa kuimba wimbo wa Tanzania na Mrisho Mpoto kabla ya kuanza 
kuonyesha fursa kupitia sanaa yake ya muziki.
Msanii
 wa kughani mashairi, Mrisho Mpoto akiwaimbisha wimbo wa Tanzania wakazi
 wa Morogoro muda mfupi kabla ya kuanza kutoa njia za kutumia fursa 
kupitia sanaa ya muziki.Semina hiyo ilifanyika mapema leo katika Ukumbi uliopo katika Hoteli ya Midland mjini Morogoro, ambapo baadhi ya wataalam kutoka sehemu mbalimbali walipata muda wa kuzungumza na wakazi hao na kuwajenga kwa kuwaonyesha njia mbalimbali za kujikwamua kimaisha.
(HABARI/PICHA:MUSA MATEJA/GPL, MOROGORO)

No comments:
Post a Comment