Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.
Sophia Simba wakati akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu
wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi
ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO-Dar es Salaam.
SERIKALI imeshtushwa na baadhi ya
ujumbe wa maneno uliopelekwa kwa wananchi na baadhi ya vyama vya siasa
hapa nchini ambao unaweza kuleta kuhatarisha amani na usalama wa
Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Wizara
ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba leo jijini Dar es
salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake.
Waziri Simba amesema kuwa kauli
zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya vyama vya siasa vilivyofanya
mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani zimeishtua Serikali na
zinaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii hususani wanawake, wazee,
walemavu na watoto.
Waziri Simba amesema kauli
zilizotolewa na viongozi hao ni pamoja na "Vijana msikubali wakati wa
kufanya mazoezi umefika" kauli hii inahitaji tafakari na kuhoji kwa
makini inawahamasisha vijana kutii, jambo ambalo linaweza kuwafanya
walete vurugu..
Amesema kuwa kauli hiyo na nyingine
zilizotolewa na viongozi hao wa juu wa vyama hivyo zinazowachochea
wananchi kutotii na ni ishara ya uwepo wa njama mbaya za kuwashawishi
wananchi ili siku hiyo wajichukulie sheria mikononi, kinyume cha katiba,
sheria na haki za binadamu.
Aidha, Waziri Simba alisema jamii inahitaji kutafakari juu ya kauli hizo na mustakabali wa Tanzania.
Amesema kuwa jamii ya Watanzania
inatakiwa kutambua kuwa amani na usalama ndio mtaji namba moja wa
maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Ustawi wa jamii ya
Watanzania unahitaji amani, utulivu na usalama.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment