




• Airtel yakabidhi vitabu kwa shule za sekondari Bihawane, Kibakwe, Itiso na Ndido mkoani Dodoma
Katika muendelezo wa kuhakikisha inatoa huduma zilizo bora kwa jamii nzima, Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu imefanikiwa kutoa vitabu vya kiada kwa shule mbalimbali zilizopo katika manispaa ya Dodoma.
Katika muendelezo wa kuhakikisha inatoa huduma zilizo bora kwa jamii nzima, Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu imefanikiwa kutoa vitabu vya kiada kwa shule mbalimbali zilizopo katika manispaa ya Dodoma.
Miongoni mwa shule zilizonufaika na mradi huo ni pamoja na Bihawane,
Kibakwe, Itiso na Ndido zote zikiwa ni shule za sekondari katika mkoa
huo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu hivyo, Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi alisema vitabu hivyo vitatumika
kuendeleza elimu katika mkoa huo na kuwakwamua wengi katika utumwa wa
kifikra.
“Udhamini huu wa Airtel utasaidia maendeleeo ya sekta ya
elimu katika mkoa wetu wa Dodoma na kusaidia wanafunzi wengi waweze
kuvutika katika usomaji wa vitabu mbalimbali kujikomboa na ujinga na
umaskini ambao umekuwa ni tatizo kubwa sio tu kwa Dodoma bali kwa nchi
nzima”.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Airtel kuchangia elimu nchini
Meneja Mauzo wa Kanda Bw, Stephe Akyoo Alisema “Airtel inatoa vitabu
hivi katika dhumuni la kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinainuka na
kuleta ukombozi wa kiuchumi na kimaendeleo kwa jamii na nchi kiujumla”.
Nae Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bihawana Dodoma Crispin Mtesigwa
alisema “Tunashukuru Airtel kwa kutoa vitabu hivi kwa shule mbalimbali
za sekondari hapa nchini na huo ni mchango dhahiri wa maendeleo kwa nchi
nzima. Ni jukumu letu sisi walimu na wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi
vilivyotolewa na Airtel vinatumika kama ilivyokusudiwa”
Kupitia mradi huo wa shule yetu, mpaka sasa shule zaidi ya 1,000
zimeweza kunufaika na mradi huo kwa kujipatia vitabu vya kiada hasa
kwenye masomo ya Fizikia, Hisabati, kemia na Biolojia. mradi huu wa
Shule yetu unasambaza vitabu kwa shule za sekondari kuanzia kidato cha
kwanza mpaka cha nne pamoja na vitabu vya walimu kwa ajili ya
kufundishia.
No comments:
Post a Comment