WAWEZA
kusema lolote kuhusu Arsenal kwa sasa, lakini kubwa ni kwamba iko
vizuri. The Gunners leo wameua 4-1 Norwich Uwanja wa Emirates na kupanda
kileleni mwa Ligi Kuu ya England, utamu zaidi ni bao la Jack Wilshere
ambalo moja kwa moja linaingia kwenye kinyang'anyiro cha bao bora la
msimu.
Wilshere
alifunga dakika ya 18, mchezaji ghali wa Arsenal, Ozil akafunga mawili
dakika ya 58 na 88 na lingine Ramsey dakika ya 83, wakati la Norwcih
lilifungwa na Howson dakika ya 70.
Kikosi
cha Arsenal ilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs,
Arteta, Flamini/Ramsey dk37, Wilshere, Ozil, Cazorla/Rosicky dk59 na
Giroud/Bendtner dk78.
Norwich: Ruddy, Martin, Turner, Bassong, Olsson, Tettey/Hoolahan dk79, Snodgrass,Howson, Fer, Pilkington/Redmond dk70 na Hooper.
Anamalizia: Wilshere alifunga baada ya gonga safi
Bao la msimu: Wilshere akifunga bao tamu
Furaha tupu: Olivier Giroud akishangilia na Wilshere
Kugombea mpira: Sebastien Bassong akipamabana na Giroud
Ruka juu: Giroud, akienda hewani kuwania mpira wa juu
Kichwa kwanza: Mesut Ozil akiifungia bao pili Arsenal
Kiulaini: Ozil akishangilia bao lake Arsenal
La kufutia machozi: Jonny Howson aliifungia Norwich la kufutia machozi
No comments:
Post a Comment