Na Boniface Wambura, Ilala
BAO pekee la Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 67 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Azam, imepanda kileleni baada ya kutimiza pointi 20 kutokana na mechi 10, wakiizidi pointi mbili Simba SC iliyocheza mechi tisa.
Lakini Azam inaongoza ligi hiyo kwa wastani wa mabao tu, kwani Mbeya City iliyoifunga JKT Ruvu 1-0 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya bao pekee la Jeremiah John dakika ya 36 nayo imetimiza pointi 20, hivyo inazidiwa wastani wa mabao na timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa.
Azam kileleni Ligi Kuu |

Katika
mechi nyingine za leo, Ashanti United imegawana pointi na Ruvu Shooting
baada ya sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Mabao ya
Ashanti yalifungwa Tumba Swedi dakika ya nane kwa penalti na Mussa
Nampaka dakika ya 88, wakati ya Ruvu yote yalifungwa Elias Maguri dakika
za 24 na 49.
Mtibwa
Sugar imeifumua 4-1 Mgambo JKT Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro,
mabao yake yakitiwa kimiani na Shaaban Nditi dakika ya 17, Juma Luizio
dakika ya 25 na 60 na Salum Mkopi dakika ya 61, wakati la Mgambo
lilifungwa na Malimi Busungu dakika ya 83.
Kagera Sugar imeilaza 1-0 Coastal Union Uwanja wa Kaitaba, Bukoba bao pekee la Salum Kanoni kwa penalti dakika ya 58.
CREDIT BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment