Mwanadada aliyerudi kwa kasi kwenye gemu la muziki nchini na kuachia ngoma zake mbili kali sana mwaka huu “Squeeze it” na “Summer Holiday”,
Baby madaha, ameendelea kudhihirisha kuwa mwaka huu kajipanga Zaidi
kusaka hela baada ya hivi karibuni kuachia Perfume na Mifuko yenye jina
lake (Brand) huko nchini Kenya.
Akizungumza kwa simu tokea nchini humo ambako yupo akijiindaa
kufanya tour yake ya kwanza baada ya kupata Mkataba na Kampuni ya Candy n
Candy records ya nchini humo, Baby Madaha amsema perfume hizo
zimeshaanza kuuzwa na kupatikana katika mitaa na maeneo mbalimbali ya
nchi hiyo na amesema kuwa mzigo wa pili utatua Tanzania hivi karibuni.
“Nimeona bora nianze na Kenya kwanza kwasababu nimegundua kuwa
huku nina mashabiki wengi sana Zaidi hata ya bongo, hata siamini
kinachotokea” Alisema baby Madaha.
No comments:
Post a Comment