KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Paskasi
Muragili, amesema kuwa mpango wa kuwavunjia wananchi nyumba
zilizojengwa katika maeneo yasiyopimwa uko pale pale.
Muragili alitangaza msimamo huo jana alipokuwa akizungumza na gazeti
hili, akijibu malalamiko ya wakazi wa maeneo ya Kikuyu Kusini, Mkalama,
Imagi, Miganga, Chinyika na Kata ya Mkonze, wanaopingana na CDA kwa
kutaka kuwavunjia nyumba zao.
Kaimu mkurugenzi huyo alisema kama kweli mji wa Dodoma unatakiwa uwe
jiji, lazima ujengwe kwa ramani iliyopo ambayo imeboreshwa na si
kuruhusu ujenzi holela.
Wananchi wa maeneo hayo waliilalamikia CDA kwa nadai kuwa imekuwa mwiba kwa wakazi wa Dodoma.
Ili kuonesha kukerwa na msimamo wa CDA, wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Kata ya Kikuyu Kusini walirudisha kadi za chama hicho
mbele ya diwani wao kwa madai kuwa chama hicho hakiwajali wanyonge.
Tukio la kurudisha kadi za CCM lilitokea hivi karibuni katika mkutano
wa hadhara ambao uliitishwa na wananchi kwa lengo la kujadili hatua ya
CDA kutaka kubomoa nyumba zao.
Wananchi hao kwa nyakati tofauti katika mkutano huo, walidai kuwa
wamechoshwa na CCM kwani inawakumbatia matajiri na kuwatelekeza
wanyonge.
Hatua hiyo ya wananchi wa Kata ya Kikuyu, imetokana na barua ya CDA
kuwaandikia wananchi wa eneo hilo kusisitiza kwamba mpango wa kubomoa
nyumba zao upo pale pale
No comments:
Post a Comment