ENGLAND imeongeza matumaini ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kuifumua Montenegro mabao 4-1 usiku huu.
Mabao ya England inayofundishwa na Roy Hodgson yamefungwa na Rooney
dakika ya 48, Boskovic akajifunga dakika ya 62, Townsend dakika ya 78
na Sturridge dakika ya 90 kwa penalti, lakini la wageni limefungwa na
Damjanovic dakika ya 71.
Kikosi
cha England kilikuwa: Hart, Walker, Cahill, Jagielka, Baines,
Gerrard/Milner dk87, Lampard/Carrick dk65, Townsend/Wilshere dk80,
Rooney, Welbeck na Sturridge
Montenegro:
Poleksic, Pavicevic/Beciraj dk57, Kecojevic, Savic, Jovanovic,
Zverotic, Drincic, Boskovic, Volkov/Vukcevic dk72, Damjanovic na
Jovetic/Kazalica dk81..
Bao safi: Andros Townsend akiifungia England bao la tatu katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa
Wayne Rooney (Namba 10) akiifunai England bao la kwanza
Leighton Baines akijaribu kupasua ukuta wa Montenegro
Gerrard akipiga juu ya lango
Gerrard akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Branko Boskovic
Presha inapungua: Kocha Roy Hodgson akiangalia vijana Uwanja wa Wembley
Nayo
Ujerumani imeendeleza ubabe baada ya kuifumua Jamhuri ya Ireland mabao
3-0 usiku huu, shukrani kwao Khedira aliyefunga dakika ya 12, Schurrle
dakika ya 58 na Ozil dakika ya 90.
Sami Khedira akiifungia Ujrumani bao la kwanza
No comments:
Post a Comment