MKAZI wa Chiringe wilayani Bunda mkoani Mara, Makeremo Mangasini
(33), amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda, akidaiwa kumuua
mkewe, Rehema Makelemo.
Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyo Safina Simfukwe,
ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Masudi
Mohamed kuwa mnamo Oktoba 5 mwaka huu, majira ya saa kumi jioni, huko
katika mtaa wa Chiringe, mshtakiwa alimpiga mkewe Rehema Makelemo kwa
mateke na fimbo sehemu mbalimbali za nwili na kusababisha kifo chake.
Mwendesha mashtaka huyo aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio
mshtakiwa baada ya kumpiga mkewe alipelekekwa na majirani katika
hospitali ya DDH Bunda na muda mfupi baadaye alifariki akiwa anapatiwa
matibabu.
Masudi alifafanua kuwa chanzo cha ugomvi wao ni wivu wa kimapenzi
ambapo mume alikuwa akimtuhumu mkewe kwamba alikuwa akitoka nje ya ndoa
yao.
Hata hivyo mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote baada ya kusomewa
shtaka lake kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa
kusikiliza kesi hiyo.
Kesi hiyo itatajwa tena Novemba mosi wakati mtuhumiwa amerejeshwa rumande
No comments:
Post a Comment