Dar es Salaam.
Mshindi wa gari la kwanza katika Promosheni ya Chomoka na Mwananchi, Benedict Mgoo (59), mkazi wa Dodoma amekabidhiwa zawadi yake, huku akisema ni Mungu ndiye amemwezesha kushinda gari hilo jipya kwani asingeweza kulinunua kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kusomesha watoto.
Mshindi wa gari la kwanza katika Promosheni ya Chomoka na Mwananchi, Benedict Mgoo (59), mkazi wa Dodoma amekabidhiwa zawadi yake, huku akisema ni Mungu ndiye amemwezesha kushinda gari hilo jipya kwani asingeweza kulinunua kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kusomesha watoto.
Mgoo, ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dodoma ameshinda gari aina ya Tata Vista lenye thamani ya Sh30 milioni.
Alisema ni mara yake ya kwanza kupata gari jipya kwani gari analomiliki kwa sasa ni Escudo Suzuki ambalo alinunua likiwa limetumika (used).
Hafla ya makabidhiano ya gari kwa Mgoo ilifanyika jana katika Ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) zilizopo, Tabata Relini, Dar es Salaam, ambako pia washindi wengine saba wa shindano la Chomoka na Mwananchi walikabidhiwa hundi zao za Sh 1 milioni kila mmoja.
Akimkabidhi funguo za gari hilo kwa Mgoo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MCL, Tido Mhando alimpongeza mshindi huyo ambaye aliambatana na mkewe, Fortunata na watoto wake watatu waliokuwa na furaha.
Mhando alisema shindano hilo limeandaliwa ikiwa ni
sehemu ya kuwahamasisha na kuwashukuru wasomaji wa gazeti la Mwananchi
ambao wamelifanya kuwa namba moja nchini, hivyo kuiwezesha kampuni
kuendelea kufanya vizuri na kuhakikisha inaendelea kushirikiana na
wananchi kwa karibu zaidi kupitia promosheni hiyo.
“Napenda nitumie fursa hii kuwashukuru wasomaji wetu kwamba licha ya dhahama ya kufungiwa gazeti tuliyoipata lakini tulipotoka siku ya Ijumaa, gazeti lilinunuliwa kwa wingi, hivyo kuwa faraja yetu, nasi kwa kutambua umuhimu wenu tunafikiria kuongeza gari lingine la nne ili mshindane kulipata,” alisema Mhando.
Meneja Masoko wa MCL, Bernard Mukasa, alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wasomaji kujitokeza kushiriki shindano hilo linaloendelea ili waweze kujishindia mamilioni ya shilingi kipindi hiki kilichobaki
Mgoo ambaye aliibuka mshindi katika droo ya 31 iliyochezeshwa katika ofisi za MCL, alisema ushindi huo ni faraja na umempa furaha katika historia ya maisha kwa kuwa ameshashiriki mashindano kwa nyakati tofauti hajawahi kushinda.
Washindi wengine waliokabidhiwa hundi na makazi yao kwenye mabano ni Stephen Mbata (Tegeta), Peter Mahinya (Tabata), Mashaku Msuya (Buguruni), Levina Nyambo (Mabibo), Cletus Mubezi (Temeke),Benedict Masija (Kigamboni),Edna Maro (Tegeta) na Dk Andrew Lwali.
Katika droo ya 41 ya Oktoba 14, mwaka huu, aliyeibuka mshindi ni Athuman Killo fundi seremala na mkazi wa mjini Morogoro.
No comments:
Post a Comment