Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwa raia
wa nchi hiyo Rais Kikwete amesema hatua hiyo inafuatia mazunguzo baina
ya viongozi hao wawili yaliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda .
Japo
hajataja ni kwa namna gani mgogoro huo uliokuwa umefukuta baina ya
Tanzania na Rwanda utakuwa umepatiwa ufumbuzi, Rais Kikwete amesema
hatua ya mazungumzo baina yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame ndio chanzo
cha mafanikio hayo yote.
Tanzania na Rwanda zilingia katika mgogoro wa
kidiplomasia hadi kufikia hatua ya kutunishiana misuli kisiri baada ya
Rais Jakaya Kikwete kuzishari nchi za Rwanda na Uganda kuzungumza na
waasi wa nchi zao waliopo nchini Jamuhuiri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Jambo hilo lililopingwa vikali na Rwanda kwa
madai kwamba Rais Kikwete aliingilia mambo ya ndani ya Rwanda kwa
kuwashauri kufanya mazungumzo na watu walioua raia wa nchi hiyo.
Mgogoro huu ulipamba moto na hata kukolezwa zaidi na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Rais Kikwete ametoa wito kwa vyombo vya habari,
wanasiasa pamoja na mitandao ya kijamii kusaidia kwa upande mwingine
kuziba ufa wa uhusiano uliojitokeza kati ya nchi hizo mbili.
Aidha katika hotuba rais Kikwete alitumia fursa
hiyo kutoa ufafanuzi wa opereshi ya kuwaondoa wahamiaji haramu nchini
humo iliyofanyika hivi karibuni ambapo amesema kuwa operesheni hiyo
iliendeshwa bila kukiuka haki za binadamu.
Kuhusu wahamiaji waliokaa nchini Tanzania muda
mrefu Rais Kikwete amesema watu hao sasa watepewa uraia rasmi wa
Tanzania ili wafuate uratibu.
No comments:
Post a Comment