SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam, kupitia kwa mkuu wa mkoa
wake, Said Meck Sadiki, imekiri kuwa eneo la klabu ya Yanga limevamiwa
na sasa imewataka wavamizi hao kuondoka mara moja.
Sambamba na hilo, mkuu huyo wa mkoa ameiagiza Yanga ilipwe fidia ya eneo la barabara inayojengwa kiwango cha lami kutoka Kigogo kupitia makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga, Dar es Salaam.
Jana Jumatano, saa nne asubuhi, mkuu huyo wa mkoa akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na maofisa wa mipango miji, walifika makao makuu ya klabu hiyo kukagua eneo hilo na kugundua sehemu iliyopita barabara inayojengwa imeingia kwenye eneo la Yanga na pia kuna watu wamevamia eneo hilo na kujenga.
“Alama zinaonyesha barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami imeminya sehemu ya eneo la Yanga, lakini hawakufidiwa na kisheria inabidi wafidiwe. Pia wale waliovamia eneo la Yanga inabidi waondoke mara moja,’’ alisema.
“Nimewaambia Yanga kama kweli wana nia ya kujenga uwanja basi wawasiliane na watu wa mipango miji ili wawashauri, wawasiliane pia na NEMC, wakague kama eneo wanaloomba linafaa kwa matumizi wanayotaka au la, pia waombe kibali manispaa, huu mradi wao inabidi uzihusishe idara nyingi, waombe upya vibali ili vishughulikiwe mara moja.”
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema eneo ambalo Yanga wanalo pamoja na lile lililovamiwa na watu ni kubwa na la kutosha kujenga huo uwanja wao wa kisasa kwa mujibu wa ramani yao ambayo ameiona.
“Eneo ni kubwa ila kama watataka eno la ziada itabidi wafuate taratibu kwa maombi rasmi na waelekeze eneo wanalotaka ili mambo yaanze kushughulikiwa,” alisema.
Awali mkuu huyo wa mkoa aliwataka Yanga kuwasiliana na ofisi ya Manispaa Ilala ambako Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Severin Assenga, alisema Yanga hawawezi kupewa eneo la ziada Jangwani kwa vile eneo wanalotaka ni la wazi.
“Hakuna nafasi ya ziada Jangwani ambayo wanaweza kuongezewa, eneo lililobaki ni maalumu kwa ajili ya michezo na mikutano mbalimbali,” ndivyo Assenga alivyokariririwa kusema.
Kuhusu barua za Yanga ambazo walidai wameiandikia ofisi yake, Assenga alisema: “Sikumbuki kama nimewahi kuona barua ya Yanga, ofisi yangu inapokea barua 200 kwa siku, siwezi kukumbuka mara moja.”
Kauli ya Assenga ilikuja baada ya uongozi wa Yanga kudai kuwa umekwama katika ujenzi wa uwanja wao baada ya kukosa kibali kutoka serikalini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Uwanja wa Yanga,
Francis Kifukwe, alisema kuwa uongozi wake uliandika barua mara mbili
zenye kumbukumbu namba YAC/Ardhi/MWA/46/2012 na ile ya YAC/Ardhi/MWA/
47/ 2012 na mpaka sasa hawajajibiwa ombi lolote.
“Mwezi wa saba mwaka huu tuliandika kwa mkuu wa mkoa lakini hajatujibu,
uwanja wetu ni ekari 3.6, tunahitaji mara tatu au nne zaidi.
CREDIT MWANASPORTS
No comments:
Post a Comment