Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipata maelezo
kutoka kwa mhandisi wa usafirishaji wa njia kuu za umeme Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini Magharibi Stanslaus Deogratias mara alipotembelea
kituo kidogo cha kuzalisha umeme cha Sumbawanga chenye uwezo wa kuzalisha megawati 5.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akitoa maelekezo kwa
watendaji wa kituo cha kuzalisha umeme cha Sumbawanga mara alipotembelea
kituo hicho.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Sumbawanga (hawapo pichani) mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika wilaya hiyo. Waziri Muhongo amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa malengo ili kuchangia katika historia ya ukuaji uchumi kwa kutegemea nishati ya umeme.
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Sumbawanga wakifurahia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya
pamoja na watendaji na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)
mara baada ya kumaliza kikao na wafanyakazi hao.
No comments:
Post a Comment