Polisi wa Misri wamefyatua moshi wa kutoza machozi
kuvunja maandamano mjini Cairo, ya wanafunzi wanaomuunga mkono rais wa
zamani, Mohamed Morsi.
Mawe yalirushwa na pande zote mbili huku
wanafunzi mia kadha wakijaribu kutoka chuoni kuelekea Medani ya Rabaa,
pahala pa kambi ya wafuasi wa Morsi ambayo ilifungwa na wakuu miezi
miwili iliyopita.
Hii ni siku ya pili ya mapambano katika Chuo
Kikuu cha Al-Azhar, ambako kuna wafuasi wengi wa chama cha Muslim
Brotherhood cha Bwana Morsi.Bwana Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwezi wa Julai.
No comments:
Post a Comment