Young
Africanimeendeleza wimbi la ushindi na kuvunjwa mwiko katika michezo
ya Ligi Kuu ya Vodacom nchini baada ya kuichpaa timu ya Kagera Sugar
mabao 2-1 mchezo uliofanyika dimba la Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kikosi cha Young Africans leo kiliingia uwanjani kwa lengo la kusaka
ushindi kwani ilikuwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo miwili mfululizo
ya Ligi Kuu katika uwanja huu wa Kaitaba.
Mrisho Ngassa alikuwa
wa kwanz kuipatia timu yake ya Yanga bao la kwanza dakika ya pili ya
mchezo kwa kichwa akimalizia mpira uliorushwa na Mbuyu Twite na kuwapita
walinzi na mlinda mlango wa Kagera Sugar na kumkuta mfungaji
aliyeukwamisha wavuni bila ajizi.
Yanga iliendelea kulishambulia
lango la Kagera Sugar kupitia kwa washambuliaji wake
Didider Kavumbagu,
Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza na dakika ya 25 nusura Niyonzima aipatie
Yanga bao lakini shuti lake liliokoloewa na mlinda mlango Aganthony
Antony na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, wenyeji Kagera Sugar 0 - 2 Young Africans.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 47 ya mchezo kiungo Boniface
Wambura aliipatia Kagera Sugar bao la kusawazisha baada ya mpira
uliopigwa na Themi Felix kuokolewa na walinzi wa Yanga na kumkuta
mfungaji.
Mara baada ya bao hilo Yanga iliendelea kulishambulia
lango la Kagera Sugar kusaka bao la pili na ushindi huku waamuzi
wakishindwa kutoa maamuzi mazuri kwani mipira yote kipindi cha pili
washambuliaji wa Yanga walionekana wameotea hata kama ni katikati ya
uwanja.
Dakika ya 57 Hamis Kiiza aliipatia Young Africans bao la
pili na la ushindi baada ya mpira uliopigwa na Mbuyu Twite kuwapita
walinzi wa Kagera na kumkuta Kiiza aliyewazidi wepesi na kuachia shuti
kali lililotinga moja kwa moja wavuni.
Yanga iliendelea kusaka bao
la tatu lakini walinzi wa Kagera Sugar waliokoa mipira ya hatari na
kufanya ubao wa matokeo uendelee kusomeka hivyo hivyo.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, wenyeji Kagera Sugar 1 - 2 Young Africans
Kikosi
cha Young Africans mara baada ya mchezo wa leo, kesho kitaondoka mjinii
Bukoba kurejea jijini Dar es salaam tayari kwa kuanza maandalizi ya
mchezo unaofuata dhidi ya Simba SC tarehe 20-10.2013 uwanja wa Taifa.
Young Africans:
1.Barthez, 2.Twite, 3.Luhende, 4.Cannavaro, 5.Yondani, 6.Chuji,
7.Niyonzima/Msuva, 8.Domayo, 9.Kavumbagu, 10.Ngassa, 11.Kiiza/Javu
No comments:
Post a Comment