Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali akiwashukuru wageni waalikwa wakiwiwemo Waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi mbalimbali kutoka bara la Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwa kufika kwao kwenye chakula cha jioni Fairmont Hotel iliyopo Washington, DC walichomuandalia mwanamuziki maarufu kutoka Afrika ya Kusini, Yvonne Chaka Chaka kwa heshima ya kuwa Balozi wa kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa malaria Barani Afrika. Balozi Amina Salum Ali aliwashukuru Benki ya Dunia kwa juhudi za makusudi wanazofanya kuhakikisha Bara la Afrika linatokomeza kabisa gonjwa hili hatari la Malaria, pia Balozi Amina Salum Ali alimshukuru Bwn. Tim Ziemer kutoka USAID kwa jitihada zao za kupigana kuutokomeza ugonjwa wa malaria Duniani hususani Bara la Afrika.
Kushoto ni Mwanamuziki wa Afrika ya Kusini Yvonne Chaka Chaka akifuatilia hotuba ya Balozi wa African Union Mhe. Amina Salum Ali, kulia ni Kaimu Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Marekani Mhe. Johnny Moloto.
Kutoka kushoto ni Mhe. Balozi wa Swaziland Rev. Dr. A. M. Ntshangase, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Balozi wa Botswana nchi Marekani Mhe. Dr.Tebelelo Mazile Seretse.
Dr. Anne Maryse B. Pierre-Louis ambaye ni mkuu wa utawala na mtaalam wa maswala ya afya kutoka Benki ya Dunia akielezea jitihada za Benki ya Dunia inazofanya kupigana kuutokomeza ugonjwa wa Malaria Barani Afrika. Pia alimshukuru mwanamuziki kutoka Afrika ya Kusini, Yvonne Chaka Chaka kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwa Balozi wa kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria Barani Afrika.
Dr. Anne Maryse B. Pierre-Louis akimpa mwanamuziki Yvonne Chak Chaka zawadi ya maua ambayo yametoka Afrika ya Kusini.
Mwanamuziki Yvonne Chaka Chaka akimshukuru Balozi Amina Salum Ali na African Union kwa kumuandalia chakula cha usiku maalum kwa kutambua mchango wake wa kampeni ya kupigana na kuwaelimisha hasa wakina mama na watoto wa Afrika ambao ndio waathirika namba moja na gojwa hili la malaria na akaelezea sababu ya yeye kuamua kuwa Balozi wa kampeni hii ni siku mmoja wa wanamuziki wake alipokufa kutokana na malaria ndipo aliguswa na kuamua kuwaelimisha wanawake wenzake hususai waishio vijijini na kazi hiyo ameifanya ipasavyo kwani mpaka hapo anapoongea ameishatembelea nchi zote za Afrika mijini mpaka vijijini kuelimisha na hatimae kuutokomeza ugonjwa huu wa malaria barani Afrika.
Tim Ziemer kutoka USAID akielezea jitihada wanazofanya kwenye kampeni ya kuutokomeza Malaria Duniani Bara la Afrika likiwa limepewa kipaumbele.
Mhe. Liberata Mulamula akichangia hoja ya malaria kwa kuelezea jitihada za Tanzania akiwemo Rais Jakaya Kikwete za kupigana mpaka mwisho na kuhakikisha malaria Tanzania inatokomezwa kabisa pia Balozi Mulamula aliezea jitihada zilizofanywa na serikali ya kuutokomeza malaria Zanzibar lakini changamoto kubwa Serikali inayokabiliana nayo ni Tanzania Bara ambako malaria bado ipo.
Kutoka kushoto ni Dr. Anne Maryse B. Pierre-Louis wa Benki ya Dunia, Mhe. Balozi wa Rwanda nchini Marekani Prof. Mathilde Mukantabana, mwanamuziki toka Afrika ya Kusini Yvonne Chaka Chaka, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Balozi wa African Union nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali katika picha ya pamoja.
Juu na chini ni Mabalozi kutoka nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani, Balozi wa African Union na mwanamuziki kutoka Afrika ya Kusini Yvonne Chaka Chaka katika picha ya pamoja.
Mabalozi kutoka nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani, Balozi wa African Union na mwanamuziki kutoka Afrika ya Kusini Yvonne Chaka Chaka wakiwa kwenye meza ya chakula picha na Vijimambo Blog
No comments:
Post a Comment