RAIS
mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ameitwa ili
kukaa na kujadiliana na shirikisho la hapa, KFF, ili kuboresha nguvu ya
maendeleo katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Rais wa
Shirikisho la Soka Kenya (KFF), Sam Nyamweya, amesema anaamini Malinzi
ni kati ya watakaochangia kasi ya maendeleo ya soka katika ukanda huu.Akizungumza Jumatatu nyumbani kwake jijini hapa, Nyamweya alisema Malinzi ni kati ya watu anaoamini ni wachapakazi.
“Tayari
nimeandaa utaratibu ikiwezekana nikutane na Malinzi, tujadili masuala
kadhaa kwa ajili ya maendeleo pamoja kama nchi za Afrika Mashariki na
baadaye nitafanya hivyo kwa Uganda, Rwanda na Burundi.
“Inawezekana kabisa kufanya kitu vizuri mkiwa pamoja, kila upande utafanya juhudi kuendeleza sehemu husika na baada ya hapo tunachangia kama ukanda wetu.
“Inawezekana kabisa kufanya kitu vizuri mkiwa pamoja, kila upande utafanya juhudi kuendeleza sehemu husika na baada ya hapo tunachangia kama ukanda wetu.
“Itakuwa
kazi ngumu sana kuendelea na kushindana na Kaskazini na Magharibi mwa
Afrika kama tutaendelea kutengana na kila mmoja anafanya mambo yake tu,”
alisema Nyamweya.
“Hata kama kuna tatizo na tunaona Caf
wanatusumbua au kuna kitu kinatukandamiza, inaweza kufikia wakati
tukapiga kelele pamoja na kupinga.”Alisema kuhusiana na mwaliko wa Malinzi, atawasiliana naye na kuangalia lini atakuwa na nafasi naye pia lini ana nafasi, halafu atalifanyia kazi.
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment