Na Wilbert Molandi
WAPO sokoni! Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa wachezaji 14 wa Yanga ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), mchezaji anapobakiza miezi sita kwenye mkataba, anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine inayomhitaji, kama ilivyo kwa wachezaji hao 14 wa Yanga ambao unaweza ukasema wapo sokoni.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya kamati ya usajili ya timu hiyo, tayari uongozi wao umeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji unaohitaji kuwabakiza.
Chanzo hicho kiliwataja wachezaji wanaotarajiwa kumaliza mikataba kuwa ni Ally Mustapha ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani na Ibrahim Job.
Wengine ni; Athumani Idd ‘Chuji’, Frank Domayo, Simon Msuva, Salum Telela, Didier Kavumbagu, Jerry Tegete na Said Bahanuzi.
“Tayari tumeshaanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji tunaowahitaji waliobakiza miezi miwili kwa ajili ya kuwaongezea,” kilisema chanzo hicho.
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment