NYUMA ya sakata la mwanamke, Violet Mathias, mkazi wa PPF jijini hapa
aliyepigwa risasi begani na polisi baada ya kukaidi amri ya kutopaki
gari sehemu isiyoruhusiwa katika Benki ya CRDB Jengo la TRA hivi
karibuni, limeibua mambo mapya nyuma ya pazia.
Ilidaiwa kuwa, polisi alimuwahi mwanamke huyo baada ya yeye kuchukua
bastola kwenye gari na kuikoki tayari kumfyatulia, akapigwa yeye
mkononi.
Habari nyuma ya pazia zilidai kuwa, siku hiyo haikuwa mara ya kwanza
kwa mwanamke huyo na watu wengine kuzuiwa kupaki sehemu hiyo ambayo ina
mlango wa kuingilia mkono wa kushoto wa Jengo la Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) ambapo ndani yake kuna Benki ya CRDB.
Toyota
Cresta lenye namba za usajili T888 BWW mali ya Vailet Mathias
lililotolewa upepo na kusababisha ugomvi baina ya Polisi na mmiliki huyo
aliyepigwa risasi begani.
Ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, Violet alipaki tena gari
eneo hilo na alipofuatwa na kuambiwa akalisogeze alikataa kwa nyodo.
Ilidaiwa kuwa baada ya kunusurika kifo Violet au Vai kama
anavyojulikana jijini hapa alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Arusha ya Mount Meru ambayo ipo hatua kadhaa kutoka eneo la tukio.
Habari zilidai kuwa katika kuficha tukio hilo, Violet ambaye ni
mwanamke mrembo na mfanyabiashara wa madini na kusafirisha watalii
alihamishwa ‘kiaina’ katika hospitali hiyo na kupelekwa Hospitali ya
Seliani iliyopo jijini hapo.
Hata hivyo, katika tukio hilo lililothibitishwa na Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kumekuwa na usiri mkubwa wa waandishi
wa habari kujua wodi aliyolazwa kwa kuwa ndugu hawataki apigwe picha.
Kutokana na kuzagaa kwa silaha mkoani hapa, jeshi la polisi limeombwa
kukusanya silaha zisizo milikiwa kihalali kutoka mikononi mwa raia ili
kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.
No comments:
Post a Comment