KATIKA hali isiyotarajiwa, staa wa sinema za Kibongo,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ amenaswa na kamera yetu akiangua kicheko cha
nguvu huku misa ya msiba ikiendelea.
Tukio hilo lililowaacha midomo wazi waombolezaji lilitokea Jumanne
iliyopita nyumbani kwa marehemu baba wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’,
Isaac Abraham maeneo ya Sinza-Mori, jijini Dar wakati Lulu alipokuwa
amekwenda kumfariji mwigizaji mwenzake huyo.


Baada ya kugundua papararazi wetu anawafotoa picha, ghafla wawili hao
walihamaki na kuacha kucheka huku wakijiziba usoni wasiweze kunaswa
sura zao kiurahisi na kamera.
Katikati ya wiki hii, Lulu aliripotiwa kuwa amevurumusha matusi kwa
mapaparazi katika msiba huohuo hali ambayo inawafanya mashabiki wahoji
kulikoni?
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment